Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imetoa maamuzi yake ya
awali kwa kumsimamisha mchezaji wa Yanga Kelvin Yondani kutokana na kitendo
chake cha kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba SC kwenye mchezo wa namba 178
uliochezwa Aprili 29, 2018.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu
wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa
habari hii leo Mei 03, 2018 jijini Dar es Salaam na kusema Uamuzi huo
umeamuliwa baada ya Kikao kilichokaliwa Mei 01, 2018 chini ya Mwenyekiti wake
Clement Sanga pindi walipokuwa wanapitia matukio mbalimbali yaliyoweka
kujitokeza katika mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Mchezaji Kelvin Yondani wa
Yanga amesimamishwa hadi suala lake la kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba
litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Adhabu ya kusimamishwa kwake
imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa
Ligi", amesema Wambura.
Kitendo cha Kelvin Yondani kumtemea
mate mchezaji mwenzake Asante Kwasi katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam
katika mchezo wa 'Kariakoo Derby' kiliweza kuamsha hisia kali kwa wapenda soko
nchini, huku wengine wakifika mbali zaidi wakizita mamlaka husika kutolifumbia
macho suala hilo kwa madai haliendani na utamaduni wa michezo.
TFF yatoa maamuzi ya Kumsimamisha Yondani kwa kumtemea mate Asante Kwasi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment