Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck
Mlinga amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kutumia nguvu
alizonazo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatukana
viongozi huku akimtaja Mange Kimambi na wengineo kama vinara.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo
ya ndani kwa 2018/19, Mlinga amemtaka IGP kutumia nguvu alizowekewa mabegani
kuwawajibisha watu wanaotukana kwani wamevuka mipaka hadi kufikia hatua ya Rais
kutukanwa.
“Matusi mitandaoni ni 'too
much', kwenye mitandao hajulikani Rais ni nani, kiongozi ni nani, kuna akaunti
nyingi zinatukana, wanatukanwa wananchi, mawaziri mpaka Rais. IGP uko hapa
tumekuwekea hizo nyota mabegani ni nguvu, tumia nguvu zako
wasikuchezee. Mfano natoa akaunti zinazomtukana rais ni kama Kwinyara,
Malisa GJ, Yericko Nyerere na Dada yao Mange Kimambi wamekuwa wakimtukana rais".
Mlinga
Aidha Mbunge huyo ameongeza "Jamani
hakuna nchi ambayo rais anachezewa. Mfano nimtolee mfano Kagame, umeshawahi
kusikia mtu anamtukana Kagame? Polisi tumieni nguvu zenu".
Mlinga ampa kazi IGP kuhusu kina Mange
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment