Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka
mitatu mkazi wa kijiji cha Keringet kaunti ya Pokot amekutwa na sindano 7 za
kushonea kwa mkono tumboni mwake, baada ya kupigwa picha ya xray.
Mtoto huyo alipelekwa hospitali ya
Kapenguria siku ya Jumanne kupata matibabu ya maumivu ya tumbo ambayo alikuwa
akiyapata kwa muda mrefu bila kujua tatizo ni nini.
Bibi yake Bi. Emily Linga'a ambaye
ndiye anayeishi naye, amesema mtoto huyo alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo
kwa zaidi ya miaka miwili, lakini hawakuweza kubaini mara moja chanzo cha maumivu
hayo na kuendelea kumpatia dawa za kutuliza maumivu, lakini baada ya kuona
anazidi kualalamika walimpeleka hospitali na kugundua ana tatizo hilo.
“Kwanza nilidhani mtoto alikuwa na
minyoo, sikuwahi kufikiria kwamba ana sindano tumboni mwake, nilikuwa nahisi ni
malaria siku zote na kumpa dawa za maumivu”, amesema bibi huyo ambaye anaishi
naye, baada ya mama yake kumuacha alipoolewa na mwanaume mwengine.
Madaktari wa hospitali hiyo wamempa
rufaa ya kwenda hospitali kubwa ya Moi ili kuwea kufanyiwa upasuaji wa tumbo,
na kutolewa sindano hizo ambazo hazijajulikana zimeingiaje.
Mtoto akutwa na sindano 7 tumboni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment