Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema
maamuzi ya Rais Dkt. John Magufuli ya kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa
ya Dodoma kuwa Jiji ni sahihi na ameyafanya kwa wakati muafaka na hakuna sheria
iliyokiukwa.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Alhamisi, Mei 3, 2018) Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 21 mkutano wa 11
wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la
Mbunge wa viti maalumu Bibi Felista Bura ambapo alitaka kupata kauli ya
Serikali juu ya baadhi ya watu wanaobeza maamuzi ya Rais Dkt. Magufuli ya
kuupandisha hadhi mji wa Dodoma.
"Rais Dkt. Magufuli hakukiuka
sheria kwa sababu ana mamlaka kwa mujibu wa katiba ibara 2 na sheria ya Mamlaka
ya serikali za Mitaa sura ya 288 kupandisha hadhi mji au eneo lolote kadiri ya
mahitaji yatakavyohitajika. Hata kitendo cha Dodoma kuwa Makao Makuu ya
Serikali pamoja na upatikanaji wa miundombinu muhimu kama ya afya, maji, umeme,
barabara na kuendelea kukua kwa ukusanyaji mapato ni vigezo tosha vya kuufanya
mji wa Dodoma kuwa Jiji", amesema
Waziri Majaliwa.
Pamoja na hayo, Waziri Mkuu
ameendelea kwa kusema "Dodoma inajitosheleza kwa mahitaji mengi
ikiwemo uwepo wa taasisi mbalimbali muhimu kama Bunge la Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania, vyuo vikuu zaidi ya vitano, Ofisi ya UN, hivyo nampongeza
Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa uamuzi wake kwani unaleta tija kwa wananchi.
Nashauri jambo hili lipongezwe badala ya kubezwa".
Aprili 26, 2018 Rais Dkt. Magufuli
aliupandisha hadhi mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa
Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la
Dodoma.
Waziri Mkuu Raisi hajakiuka sheria kupandisha manispaa ya Dodoma Kuwa jiji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment