Mbunge wa Tarime
Vijijini (CHADEMA) John Heche amesema Shirika la Umeme nchini TANESCO
halitaweza kupata faida mpaka kuisha kwa dunia kutokana na mkataba wa kifisadi
waliongia na kampuni ya uzalishaji umeme ya Songas.
Heche amesema hayo leo Mei 25, 2018
Bungeni Jijini Dodoma, alipokuwa akichangia hoja mjadala wa makadirio ya mapato
na matumizi ya Wizara ya Nishati katika mwaka wa fedha 2018/2019 na kuongeza
kuwa kama mkataba huo utaendelea basi madeni ya TANESCO yatazidi kuongezeka
maradufu.
“Mwenyekiti umesema hapa TANESCO
wameanza kupata faida, kamwe mpaka dunia hii inaisha TANESCO hawatapata
faida kwasababu mkataba walioingia na Songas ni mkataba wa kihuni na wizi
ndiyo unasababisha shirika hili kuendelea kuwa na madeni na hata dunia hii
inaisha kama mkataba na Songas utaendelea kuwepo madeni ya TANESCO yataendelea
kuwa makubwa”,amesema Heche.
Mbunge huyo ameongeza kuwa kitendo
cha TANESCO kuwa shirika pekee linalozalisha umeme nchini bila ya kuwa na
mshindani imechangia kwa kiasi kikubwa kuwa na mzigo wa kutoa huduma pamoja na
madeni ambapo mpaka kufikia sasa TANESCO inadaiwa zaidi ya bilioni 900.
Bunge limepitisha makadirio ya
mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo
jumla ya shilingi trilioni 1.69 imeizinishwa kwa matumizi ya miradi ya
maendeleo na matumizi ya kawaida.
"Tanesco haitapata faida kamwe"- Heche
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment