Mbunge Kasuku Bilago afariki dunia

Mbunge wa jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma kupitia CHADEMA, Mh. Kasuku Samson Bilago amefariki dunia mchana huu akiwa katika Hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu
 
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, ambapo ameeleza kuwa taarifa zaidi juu ya msiba huo zitatolewa muda si mrefu.

Mheshimiwa Bilago pia alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA.

chanzo EATV
Mbunge Kasuku Bilago afariki dunia Mbunge Kasuku Bilago afariki dunia Reviewed by KUSAGANEWS on May 26, 2018 Rating: 5

No comments: