Mhadhiri wa Udom alichomwa visu mara 13

Familia imeeleza kuwa Mhadhiri wa masomo ya Kompyuta, wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Rose Mndenye, alichomwa visu mara 13 shingoni

Akisimulia namna tukio hilo lilivyotokea, dada wa marehemu, Evonia Mndenye amesema mdogo wake alikutwa na matundu 13 ya visu shingoni

Akizungumza leo Mei 26 akiwa  nyumbani kwake eneo la Kisasa Sheli, mjini Dodoma, ulipo msiba,  Evonia  amesema  Rose alishindwa kujitetea kwa kuwa alikuwa yeye na mtoto wake mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu

Mwili wa Rose ulikutwa  nyumbani kwake jana saa 2 usiku na mdogo wa marehemu, Lilian Mndenye

Evonia amesema msiba huo umetokea ghafla mno kwani marehemu alifanya shughuli zake siku nzima ya jana na ilipofika majira ya saa mbili usiku ndipo walipoukuta mwili wake nyumbani kwake akiwa ameuawa

“Kabla ya kufikwa na umauti huo Rose alikuwa akiwasiliana na mdogo wao mwingine aliyejulikana kwa jina la Liliani aliyekuwa anatokea Wilayani Manyoni ambaye baada ya kufika nyumbani kwa marehemu ndipo alipokutana na mauaji hayo,” anasimulia

Evonia anasimulia zaidi kuwa wakati wa uhai wake, marehemu alikuwa akifarakana mara kwa mara na mume wake aliyetambuliwa kwa jina la John Mwaikambo

Amesema baada ya mauaji hayo kutokea mwanaume huyo amekuwa hapatikani kwenye simu yake na hata mahali alipokuwa akiishi hayupo
“Walikuwa na ugomvi mara kwa mara na mume wake alilalamika kuwa mke wake anachelewa kurudi nyumbani bila kujali kuwa Rose ni mtumishi wa serikali.” Amesema Evonia

Mdogo wa marehemu, Lilian amesema alipofika nyumbani kwa marehemu majira ya saa mbili usiku alikuta dada yake amekufa  na mwanaye mdogo alikuwa akichezea damu ya mama yake pembeni

“Niliwataarifu ndugu zangu wengine ambao walitoa taarifa polisi ambao walifika na kuuchukua mwili wa marehemu na kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Dodoma,” amesema

Maiti inatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Ludewa mkoani Njombe kwa mazishi


Mhadhiri wa Udom alichomwa visu mara 13 Mhadhiri wa Udom alichomwa visu mara 13 Reviewed by KUSAGANEWS on May 26, 2018 Rating: 5

No comments: