Mhudumu wa hoteli akutwa na sare za polisi, bastola


Mhudumu wa Hoteli ya Sleep Inn, na mkazi wa Mwananyamala kwa kopa, anashikiliwa na polisi  kwa kukutwa na sare za  polisi, silaha, cheo cha koplo na pingu

Katika taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa imesema, Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna mtu mmoja  anatumia sare za Jeshi la Polisi kuwakamata watu na kuwafunga pingu, kuwatishia bastola ili kufanikisha  kupora mali maeneo mbalimbali ya Jiji

“Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji mara moja na kuweka mtego. Mnamo tarehe 12 Mei 2018 majira ya saa nne usiku huko Mwenge Bamaga Polisi  walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo,” amesema Mambosasa katika taarifa hiyo

Mambosasa amesema baada ya kufanya naye mahojiano mtumiwa alikiri kumiliki sare na vifaa mbalimbali vya Jeshi la Polisi na kukubali kuwapeleka askari hadi nyumba anayoishi

“Baada ya kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo alikutwa na sare za Jeshi la Polisi, pingu, cheo cha koplo wa Polisi, mfuko wa kuhifadhia bastola na bastola aina ya  GLOCK 17 ambayo imefutwa namba zake za usajili ikiwa haina risasi,” amesema

Mtuhumiwa huyo ameshafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili

Mhudumu wa hoteli akutwa na sare za polisi, bastola Mhudumu wa hoteli akutwa na sare za polisi, bastola Reviewed by KUSAGANEWS on May 26, 2018 Rating: 5

No comments: