Serikali ya Uganda
inatarajiwa kuanza kulipa mishahara ya watumishi wake wa umma kulingana na siku
walizofanya kazi badala ya hakikisho la mshahara wa mwisho wa mwezi.
Mkuu wa Kitengo cha Uwajibikaji cha
Ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Prof. Ezra Suruma amesema wameanza kufunga
vifaa vya kielektroniki ambavyo vitafuatilia muda wa kuingia na kutoka kazini
kwa watumishi wa umma kwenye hospitali zote za umma na taasisi za elimu.
"Mishahara ya wafanyakazi ambao
hawatahudhuria kazini bila sababu maalum itakatwa kulingana na siku ambazo
hawakufanya kazi", amesema
Prof. Suruma
Prof. Suruma amefafanua zaidi kuwa
mfumo huo tayari umeanza kutekelezwa katika Wilaya za Kaliro, Kayunga, Buvuma,
Bulambuli, Bugiri na Bududa, Mashariki mwa Uganda kwa majaribio na kwamba
wanatarajia utaanza katika Wilaya zote nchini humo
Serikali yaanzisha mfumo mpya wa ulipaji mishahara
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment