Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amewataka wakulima wa ufuta wasikimbilie kuuza zao hilo kwa wanunuzi wasio
rasmi maarufu kwa jina la 'choma choma' bali wasubiri minada itangazwe
mwezi ujao.
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi mara baada ya
kukagua uwanja mpya wa michezo unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya
Nachingwea, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.
“Ninawasihi msikubali kuuza
kwa akina 'choma choma' bali tumieni Mfumo wa Stakabadhi za Mazao Ghalani,
tumeona mfumo huu ulivyosaidia kwenye korosho,” amesema.
“Kuna wawakilishi wa Kampuni
ya Hyseas International Investment (T) Limited ya kutoka China ambao wamekuja
hapa kuonana na uongozi wa Halmashauri. Wamesema watanunua ufuta wote uliolimwa
Ruangwa na Nachingwea, ndiyo maana ninawasihi msubiri, msikimbiile kuuza ufuta
kwa sasa,” Majaliwa.
Amesema kampuni hiyo imeahidi kuweka
vituo vya ununuzi kwenye kata za Mandawa, Nanjaru, Nangurugai, Machang’anja
hadi Mbangala ili wakulima wasihangaike kusafirisha ufuta wao. “Tunataka
mwaka huu, wakulima wa ufuta nao wapate hela nzuri,” .
Majaliwa awataka watu kuepuka 'choma choma'
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment