Mbuzi 47 wenye thamani ya zaidi ya
Shilingi milioni mbili mali ya bwana Sleyo Rashidi mkazi wa mjini Shinyanga,
wamedaiwa kufa kwa kula majani yenye sumu katika eneo la marisho Jeshini Kata
ya Kizumbi mjini hapa, sehemu ambayo mbuzi hao walikuwa wakichunga.
Imedaiwa mbuzi hao waliaanza kufa
usiku wa kuamkia leo Mei 25,2018 katika kitongoji cha Busongo Kijiji cha
Bugayambelele kata ya Kizumbi majira ya saa 10 usiku, ambapo sumu hiyo
waliokula kutoka machungoni eneo hilo la Jeshi, ilianza kuwazidi na kuanza kufa
mmoja baada ya mwingine.
Akisimulia tukio hilo mchungaji wa
mifugo hiyo Daudi Dotto, amesema ilipofika majira ya saa 10 usiku alianza
kusikia mbuzi wakilia, na alipo kwenda kwenye banda lao alikutana na mbwa huku
mbuzi 47 wakiwa wameshakufa na matumbo yao kuvimba.
“Mbuzi hawa hua na wachunga mara
zote katika eneo la Jeshini Kizumbi ambapo hua tunakatazwa, lakini kutokana na
uhaba wa maeneo ya marisho hua tunachunga hivyo hivyo kwa kuiba , na majira ya
jioni ni kazirudisha nyumbani ndipo majira hayo ya usiku wakafa
mbuzi 47,” amesema Dotto.
Naye Daktari wa mifugo wa
halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Velani Mwaluko ambaye alifika kwenye eneo
hilo, alisema katika uchunguzi wa awali amebaini mbuzi hao
wamekufa kwa kula majani yaliyopuliziwa Sumu, ambapo amechukua
baadhi ya Nyama kwenda maabara Jijini Mwanza, ili kubaini aina hiyo ya
Sumu.
Mbuzi 47 wamekufa kwa Sumu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment