Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu,
ameingia bungeni kwa mara ya kwanza leo Mei 21, 2018 tangu aachiwe kwa msamaha
wa Rais John Magufuli, Mei 10 mwaka huu
Baada ya kuingia bungeni, wabunge wa upinzani walilipuka kwa
furaha wakimshangilia huku wakigonga meza zao kwa takriban dakika mbili, hali
iliyosimamisha shughuli za Bunge kwa muda
Sugu ameingia ukumbini saa 3:20 asubuhi akiwa ameambatana na
mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Kunti Yusuph ambaye alisikika akisema:
"Leo bungeni ni Sugu tu."
Wakati anaingia, naibu waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege
alikuwa anajibu maswali ya wabunge, lakini akalazimika kunyamaza kwanza
Sugu alikwenda moja kwa moja kwa mbunge wa Mtama, Nape
Nnauye na kumpa mkono kisha kwa waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu, Jenister Mhagama na
kumpa mkono
Alielekea kwa mwanasheria mkuu wa Serikali, Dk Adelardus
Kilangi na waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George
Mkuchika akawapa mikopo.
Baada ya hapo akarudi
upande wake wa upinzani na kukumbatiana na mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph
Selasini na kwenda kukaa sehemu yake karibu na mbunge wa Tarime Mjini
(Chadema), Esther Matiko.
Mwenyekiti wa Bunge,
Andrew Change aliwaomba wabunge kutulia ili shughuli za Bunge ziendelee, huku
akiwatishia kuwa hatawapa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza
“Imetosha sasa, imetosha, haya endelea,” amesema Chenge
Katika suti yake kuna nembo inayoonyesha namba ya mfungwa
yenye taarifa za kifungo alichotumikia
Sugu atinga bungeni, asimamisha shughuli kwa muda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment