Spika wa
Bunge, Job Ndugai kwa mara nyingine jana alipinga majibu ya swali lililohusu
sukari ambalo liliulizwa kwa mara ya pili na mbunge, akisema kuwa bado
halijajibiwa
Swali hilo
liliulizwa na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Jaku Ayoub Hashim
Hashim
aliuliza swali hilo leo Mei 18 bungeni baada ya kuwa liliulizwa mwanzoni
mwa mwezi na serikal kutakiwa kulitolea ufafanuzi
Hashim
alihoji, kuna tatizo gani linalofanya sukari iuzwe bei ya juu kwa upande wa
Tanzania bara kuliko Zanzibar na akahoji Serikali inachukua hatua gani
kukomesha tatizo hilo?
Jaku pia
amesema kwa upande wa Zanzibar kipindi ambacho matumizi ya sukari kwa wananchi
yanaongezeka, Serikali inashusha ushuru wa kuingiza sukari nchini akahoji ni
kwa nini Serikali isiige mfumo huo na kupeleka unafuu kwa wananchi wa bara?
Awali, swali
hilo lilijibiwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage na majibu yake yalizua utata hadi Spika Ndugai akaagiza Serikali
kutafuna namna ya kulitolea ufafanuzi suala hilo. Pia aliagiza swali hilo
kurudiwa upya ili mbunge apate majibu yanayojitosheleza
Serikali
kupitia Waziri Mwijage ilipeleka majibu bungeni na kulitolea ufafanuzi jambo
hilo ambalo hata hivyo bado lilikuwa na sintofahamu kwa wabunge
Jana, Serikali
ilipeleka majibu ya swali hilo ambayo yalijibiwa na Naibu Waziri wa wizara
hiyo, Stella Manyanya lakini Ndugai akasema halijajibiwa kulingana na muuliza
swali alichotaka
“Ujue
waheshimiwa wabunge swali hili halijapata majibu kabisa, maana ukiangalia
lilivyoulizwa na majibu yake yalivyotolewa utaona vitu viwili tofauti, lakini
nalimaliza kwa namna hiyo, haya tunasonga mbele,” amesema Ndugai
Akijibu swali
hilo, Manyanya amesema bei ya sukari kwa gunia la kilo 50 ni Sh 101,000 hadi Sh
105,000 kwa Dar es Salaam na Sh 71,000 hadi 77,000 kwa Zanzibar
“Mapitio ya
bei hizo yanatokana na utozaji wa ushuru na kodi, na inaonekana dhahiri kuwa
kiasi cha kodi kinachotozwa kwenye gharama za mfuko wa kilo 50 Zanzibar ni
kidogo ukilinganisha na kodi inayotozwa kwa Dar es Salaam ambayo ni asilimia 25
na 18 vyote kwa pamoja,” amesema Manyanya
Spika asema bora liende
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment