Mtoto afariki kwa kulipukiwa betri ya simu


Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya msingi Sabasaba jijini Mwanza, Dotto Baraka (13) amefariki dunia baada ya kulipukiwa na betri ya simu aliyokuwa akiiunganisha na radio chakavu

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Mei 18, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea Mei 17 mtaa wa Igoma Mashariki jijini Mwanza

“Baada ya kutoka shuleni, marehemu akiwa na watoto wenzake alianza kutengeneza radio chakavu kwa kuchukua betri ya simu na kuunganisha kwenye nyanya za radio hiyo akitumia mdomo ndipo mlipuko ulipotokea na kusababisha kifo chake," amesema Kamanda Msangi

Amesema mlipuko huo ulisambaratisha mdomo, taya, meno na koo la marehemu aliyefia njiani wakati majirani wakijaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza hospitali

Kamanda  Msangi amesema wakati tukio hilo linatokea, wazazi wa  watoto hao walikuwa safarini, wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga

Amesema hakuna mtoto mwingine aliyejeruhiwa katika tukio hilo.</p></div><div><p>

Kamanda Msangi amewaomba wazazi kuwa makini wanapowaacha watoto majumbani wenyewe kwa kuwakanya kuepuka kuchezea vitu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao na mali

Mwili marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-toure kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kukabidhiwa kwa familia, kwa ajili ya mazishi

Mtoto afariki kwa kulipukiwa betri ya simu Mtoto afariki kwa kulipukiwa betri ya simu Reviewed by KUSAGANEWS on May 18, 2018 Rating: 5

No comments: