Shahidi katika kesi inayomkabili
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini, Abdul Nondo, amesema kuwa simu ya
mtuhumiwa ilikuwa inatumika kipindi alichokuwa anadai kwamba ametekwa.
Shahidi huyo ambaye amejulikana kwa
jina la Abdul Kareem anayehusika katika kitengo cha makosa ya mtandao amesema
kuwa simu ya Nondo ilikuwa ikitumika katika kipindi ambacho Mtuhumiwa alikuwa
akidai ametekwa ingawa ameshindwa kuelezea ilikuwa ikitumika na nani kwa madai
kuwa hana uwezo huo.
Akizungumza Wakili wa Abdul Nondo,
B. Jebra Kambole amesema kwamba mbali na Shahidi Abdul Kareem, Koplo John
ambaye ni mpelelezi katika kesi hiyo ametoa ushahidi wake ambao ni maelezo ya
Nondo aliyoyatoa katika kituo cha polisi Iringa.
Wakili Kambole amesema kwamba licha
ya serikali kuwa na mashahidi watano katika kesi hiyo, Juni 12-13 inategemea
kuwepo na mashahidi wengine ambao bado hawajajulikana watakuwa wangapi.
Hakimu katika kesi hiyo John
Mpitanjia ameahirisha kesi hiyo mpaka Juni 12 ambapo Mtuhumiwa Abdul Nondo
ataendelea kuwa nje kwa dhamana.
Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili
Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa
Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kuwa yupo hatarini, kosa la
pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi wa kituo
cha Mafinga Wilayani Mufindi.
Simu ya Nondo ilikuwa ikitumika alipotekwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment