Kubenea: Mbunge wa CCM atakayepinga bajeti Wizara ya Mifugo na Uvuvi, apewe mshahara wangu


Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameuweka rehani mshahara wake wa ubunge wa Mei, 2018 akitaka apatiwe mbunge wa CCM atakayesimama na kupinga bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi mwaka 2018/19, inayotarajiwa kupitishwa leo Ijumaa jioni Mei 18, 2018

Kubenea ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa bajeti hiyo , kubainisha kuwa wabunge wa CCM wamekuwa wakipitisha kwa nguvu bajeti baada ya kuitwa kwenye vikao vya ndani vya chama hicho

Baada ya Kubenea kueleza hayo, baadaye Spika wa Bunge, Job ndugai aliwatangazia wabunge  wa chama hicho tawala kuwa  watakuwa na kikao cha ndani kitakachofanyika katika ukumbi wa White House, kabla ya kurejea tena bungeni saa 10 jioni
Mara nyingi hoja za wabunge zinapokuwa moto bungeni kuhusu wizara fulani, CCM huitisha vikao hivyo vya ndani

“Mheshimiwa Spika kama atasimama mbunge yeyote wa CCM na kutaka kukwamisha bajeti hii, natangaza mshahara wangu wa mwezi huu apewe akaongezee bajeti yake, huwa mnatupiga maneno tu bila vitendo,” amesema Kubenea

Amesema ni aibu kwa Serikali kuendelea kuagiza nyama, kuku na samaki kutoka nje ya nchi wakati vitu hivyo vimejaa nchini
Kubenea: Mbunge wa CCM atakayepinga bajeti Wizara ya Mifugo na Uvuvi, apewe mshahara wangu Kubenea: Mbunge wa CCM atakayepinga bajeti Wizara ya Mifugo na Uvuvi, apewe mshahara wangu Reviewed by KUSAGANEWS on May 18, 2018 Rating: 5

No comments: