Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Job Yuston Ndugai ameonyesha kufurahishwa na umoja
waliouonyesha wabunge katika kuwaunga mkono wabunge waislamu katika kipindi
hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Akionyesha furaha yake bungeni,
Spika amesema kwamba amependa jinsi ambavyo wabunge wameonyesha umoja kwa kuvaa
stara (Hijab) huku akimpongeza Naibu Spika Tulia Ackson kaongoza kwa kwa
kufunika.
"Waheshimiwa wabunge
tunaendelea lakini kabla hatujaendelea, kwa utafiti wangu niliofanya leo watu
humu ndani wamependeza kwa kuvaa bargashia na kanzu. Hongereni sana, lakini
tukumbuke kanuni tunapovaa lazima tuvae inavyotakiwa kama kule pwani na miguuni
siyo kuvaa kiatu cha kamba, bali kobazi" Spika.
Ameongeza "Kwa upande wa
kina mama leo Hijab zimekubali. Lakini katika hijab, hijab namba moja leo
hii ni ya Naibu wangu Mhe. Naibu Spika (huku akicheka) na hii inaonyesha
utanzania wetu jinsi ambavyo sisi ni wamoja".
Spika aguswa na Hijab za Wabunge
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment