Serikali ya kupitia Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia imefunguka na kukanusha taarifa zinazosambazwa katika
mitandao ya kijamii kuwa wanafunzi ambao wazazi wao wana leseni za biashara
hawataruhusiwa kupata mkopo wa elimu kuwa sio za kweli na kuutaka uuma
kuzipuuza taarifa hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo Mei 11,
2018 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. William Ole-Nasha
wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kufuatia taarifa
zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na hoja za baadhi ya Wabunge walizotoa
bungeni kuwa leseni ya biashara inatumika kama kigezo cha kutowapa wanafunzi
mikopo hiyo.
"Hizo habari ni za uongo zenye
lengo la kupotosha jamii, kimsingi tuna taka umma wa watanzania wazipuuzie hizo
taarifa kwasababu sio za kweli. Mikopo inatolewa kwa kuzingatiwa uwezo wa mzazi
au mlezi wa mwanafunzi, kwa hiyo kinachoangaliwa ni kipato chake", amesema Ole-Nasha.
Pamoja na hayo, Naibu Waziri
Ole-Nasha ameendelea kwa kusema "vigezo vinavyotumika
vinabadilika kila mwaka kulingana na maboresho yanayofanywa ili kuendana na
wakati ambapo kwa mwaka huu mabadiliko hayo yamesaidia kuongeza wanufaika wa
mikopo elfu 10,000 zaidi kulinganisha na mwaka jana.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri
iza, Mh. William Ole-Nasha amesema mwaka huu matarajio ni kutoa mkopo kwa wanafunzi
laki moja na elfu ishirini na mbili (122,000) na kati yao elfu 30 ni wa mwaka
wa kwanza na elfu 80 ni wanafunzi wanaoendelea na masomo yao.
Serikali yatoa kanusha kuhusu bodi ya mikopo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment