Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe
(CCM), amesema mfumo wa kodi nchini umesababisha gharama za uzalishaji bidhaa
kuongezeka na kudumaza mazingira rafiki ya uwekezaji na kwamba hata miujiza
aliyokuwa akisubiri kuiona mpaka sasa haijatokea.
Bashe ametoa kauli hiyo leo bungeni
, wakati akichangia mjadala wa bajeti na kuongeza kuwa licha ya mwaka 2016
kumwambia Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara, Charles Mwijage kuwa
anasubiri aone miujiza katika wizara hiyo, hadi sasa inashangaza kuona hakuna
kilichotokea.
Mbunge huyo ameitaka Wizara
hiyo, kukutana na Wizara ya Fedha na Mipango ili kuweka mazingira rafiki ya
uwekezaji yatakayomsaidia Rais John Magufuli kutimiza ndoto ya kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.
“Muujiza wa kwanza ulikuwa ni
kuona namna gani Wizara ya Viwanda inaweza kuunganisha mambo matatu ambayo
amekabidhiwa. Rais aliamua kwa makusudi kuunganisha biashara, viwanda na
uwekezaji ili kufikia lengo la mapinduzi ya viwanda, lakini hadi leo
tunazungumzia General Tyre, Liganga na Mchuchuma. Kuna matatizo ya msingi ya
biashara lakini huoni kwenye mpango wetu namna ya kuyashughlikia,”
amesema.
Amesema licha ya Mwijage kutaja
vipaumbele vya wizara hiyo kwa mwaka 2018/19, hakuna mpango unaoonesha kuondoa
matatizo yaliyopo kwenye mifumo ya kodi, miongozo na sheria katika kufanya
biashara nchini.
Miujiza ya Mwijage yamuacha hewani Bashe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment