Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Simon Sirro ameagiza Watumishi wa jeshi hilo kufanya majukumu yao kwa
kuzingatia utii wa sheria ili kujenga umoja baina yao na wananchi.
Ameyasema hayo mara baada ya
kushiriki gwaride la kuwaaga Makamishana wa Polisi Alice Mapunda Kamisheni ya
uchunguzi wa kisayansi wa makosa ya jinai na Kamishna Mstaafu Fedha na
lojistiki Clodwig Mtweve kwenye viwanja vya chuo cha Polisi Kurasini.
IGP Sirro amesema ni wajibu wa kila
mtu kuhakikisha anakua mtiifu katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Kwa upande wao Makamishna wastaafu
kwa pamoja wamewataka watenda kazi wa jeshi hilo kutekeleza kazi zao kwa
uweledi na kujenga ukaribu na wananchi ili kubaini vitu vingi ambavyo ni msaada
kwa majukumu yao..
IGP awataka polisi kujenga umoja na wananchi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment