Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
amesema nchi ina sukari ya kutosha na kilichojitokeza ni propaganda ya watu
wasioitakia mema
Akihitimisha hoja ya bajeti ya wizara yake ya mwaka 2018/19
leo Mei 11, 2018 bungeni, Mwijage amesema tayari ameagiza Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula la Dawa Tanzania (TFDA) kuiondoa sukari
yote iliyopo bandarini
Amesema yeye ni mcha Mungu na asingependa kuona Waislamu
wanaotarajia kuingia katika mfungo wa Ramadhani wanapata shida ya kupata sukari
Waziri Mwijage amesema hakuna tatizo la sukari kwani kuna
akiba ya sukari tani 43,000 iliyopo katika stoo
“Lakini Tanzania tunatumia tani 40,000 kwa mwezi,”
amesema.
Amesema amewaagiza mameneja wa TBS na TFDA kuhakikisha tani
20,000 ya sukari iliyopo bandarini inaondolewa.
“Viwanda vya sukari
vyote bado kama wiki tatu vinaanza kuzalisha. Suala la sukari lilikuwa ni
propaganga na mimi ni ‘propagandist’ niliyesomea China,” amesema
Kuhusu mazingira ya uwekezaji, Mwijage amesema amekuwa
akipigania kuyafanya kuwa rafiki na kuwaomba wabunge wanapobaini kuwapo kwa
changamoto zozote waziwasilishe kwake na hatua zitachukuliwa
Pia, amesema amepokea maoni na ushauri wote uliotolewa na
wabunge na kuahidi kuufanyia kazi.
Mwijage aagiza tani 20,000 za sukari bandarini zitolewe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment