Waziri Manyanya apangua hoja za wabunge

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imesema itahakikisha amani inakuwapo ili kuwavutia wawekezaji wengi.

 Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Stella Manyanya amesema, “Amani ni jambo la msingi na sisi tutalifanyia kazi. Lakini amani ianze humu bungeni na kwa kuwa wote waheshiwa wabunge tunamuunga mkono Rais wetu katika uchumi wetu.”

Manyanya ameyasema hayo leo Mei 11, 2018 wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge walizozitoa wakati wakijadili hotuba ya bajeti ya wizara hiyo ya mwaka 2018/19 ya Sh143.3 bilioni

Kadhalika, Manyanya amesema tafsiri ya viwanda ni eneo ambalo shughuli ya kiuchumi hufanyika kwa lengo la kuzalisha bidhaa

“Tumeandaa kitabu chenye orodha ya viwanda vyote na viwanda ni sawa na binadamu, wanazaliwa, wanakuwa na wanakufa hivyo hivyo kwa viwanda,” amesema

Kuhusu ulipaji wa fidia kwenye maeneo ya uwekezaji, Manyanya amesema tayari kuna fedha zimetengwa za kulipa fidia akitolea mfano Ruvuma Sh2 bilioni zimetengwa

Manyanya akizungumzia Tume ya Ushindani (FCC), amesema Serikali inaendelea kushirikiana na wazalishaji mbalimbali ili kupata utambuzi mzuri wa bidhaa na kuondoa usumbufu uliopo kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano

Amesema suala la kuuza ufuta kwa kutumia stakabadhi gharani mchakato unafanyika ikiwamo kufanyika kwa kikao cha wadau hivi karibuni jijini Dodoma


Waziri Manyanya apangua hoja za wabunge Waziri Manyanya apangua hoja za wabunge Reviewed by KUSAGANEWS on May 11, 2018 Rating: 5

No comments: