Serikali imesema tangu
kuanza kwa matumizi ya sheria ya makosa ya mtandao namba 14 ya mwaka 2015,
imesaidia kupunguza makosa ya mtandao na upatikanaji wa haki pale mtu
anapotenda kosa tofauti na awali hivyo hawana mpango wowote kwa sasa kufanya
marekebisho kwenye sheria hiyo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mei 21,
2018 na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa
Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 33 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza la Mbunge wa Ubungo
Said Kubenea aliyetaka kujua lini serikali itapeleka bungeni mswada wa
marekebisho ya sheria mtandao inayobana uhuru wa mwananchi kupata habari.
"Uwepo wa sheria ya makosa ya
mtandao Na. 14 ya mwaka 2015 umesaidia kupungua kwa makosa ya kimtandao,
upatikanaji wa haki pale mtu anapotenda kosa kwani kabla ya hapo kulikuwepo na
changamoto na uanishaji wa makosa na adhabu hali iliyopelekea haki
kutopatikana", amesema
Kwandikwa.
Pamoja na hayo, Kwandikwa ameendelea
kwa kusema "uwepo wa sheria hiyo umewezesha kuimarika kwa
matumizi salama ya mtandao na kuleta maendeleo kwa wananchi. Sheria hii ni
muhimu sana kwa nchi yetu na badala ya kuwaathiri watumiaji au wananchi
imesaidia kupunguza waharifu wa mtandao.....
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Jeshi la Polisi inaonyesha kupungua kwa makosa hayo kwa asilimia 48.9 kati ya
Januari hadi Disemba 2017. Hivyo kwa sasa serikali haina mpango wa kupeleka
marekebisho ya sheria hiyo bungeni hadi hapo kutakapokuwa na uhitaji wa kufanya
hivyo".
Kwa upande mwingine, Kwandikwa amewataka
wananchi kutumia fursa chanya zitokanazo na matumizi sahihi ya mitandao kuliko
kutumia mitandao hiyo kuvunja sheria za nchi na maadili pamoja na tamaduni za
kitanzania.
Serikali yakataa kurekebisha sheria ya mtandao
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment