Serikali imesema
haitaweza kupanga ada elekezi kwa shule ambazo zinamilikiwa na watu binafsi
nchini bali itasimamia ubora katika uendeshwaji wa shule hizo ili kusaidia
wanafunzi wote nchini wanapata elimu bora.
Hayo yamesemwa leo Mei 21, 2018
Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
William Tate Ole-Nasha na kutoa ushauri kwa wazazi au walezi kuchagua shule
ambazo wanauwezo wa kumudu gharama ili kuepuka usumbufu kwa wanafunzi na
wamiliki wa shule hizo.
“Serikali haitajihusisha na upangaji
wa ada kwa shule binafsi bali itasimamia viwango vya ubora, taratibu, kanuni na
sheria za uendeshwaji wa shule zote nchini lengo la serikali ni kuhakikisha
watoto wote wakitanzania wanapata elimu bora kwa manufaa yao na ya Taifa kwa
ujumla”,amesema Ole-Nasha.
Kwa upande mwingine Naibu Waziri
huyo amesema kwamba kwa wanafunzi ambao watasoma katika shule binafsi wanakuwa
na nafasi ndogo ya kupata mkopo wa elimu ya juu kwasababu wanachukuliwa ni watu
wenye uwezo kwakuwa baadhi ya shule za binafsi zinagharama kubwa kuliko ada ya
Chuo Kikuu.
Mpaka sasa Nchini Tanzania kuna
jumla ya shule za msingi 1432 ambazo zinamilikiwa na watu binafsi na shule za
sekondari ni 1250.
Serikali haitapanga ada kwa shule binafsi - Ole
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment