Waziri mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amesema kuwa imani ya dini yoyote
ni lazima iendane na maendeleo ya watu ni mambo mawili ambayo hayawezi
kutenganishwa kwa maslahi ya Taifa.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo
jana Mei 20, 2018 Jijini Dodoma katika ibada maalumu ya kumtawaza Askofu Dkt.
Maimbo Ndolwa kuwa Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Tanzania na
kuongeza kuwa ni jukumu la viongozi wa dini ni kuhimiza waumini kufanyakazi kwa
bidii
“Imani ya dini na maendeleo ya watu
haviwezi kutenganishwa, kwa maana hiyo hutuwezi kutenganisha imani ya dini na
changamoto kubwa zinazotukabili ikiwemo, umaskini, maradhi na ujinga kwa namna
nyingine umaskini huletwa na watu kutofanyakazi ni vizuri tuhimize waumini wote
kufanyakazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kuondoa umaskini”, amesema Majaliwa.
Kwa upande mwingine Waziri Mkuu
Majaliwa aliwasisitiza viongozi wa dini nchini kuendelea kuliombea Taifa la
Tanzania na viongozi hasa Rasi Dkt John Magufuli ili awe na busara, hekima,
upendo na hekima katika kuiletea nchi maendeleo.
Askofu Dkt. Maimbo Ndolwa alitawazwa
kuwa Askofu Mkuu wa saba wa kanisa la Anglikana nchini Tanzania katika ibada
iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika
Jijini Dodoma
Hatuwezi kutenganisha dini na maendeleo - Majaliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment