Askofu Mkuu Mteule wa
Kanisa la Anglikana nchini, Askofu Maimbo Mndolwa amesema wao kama Kanisa wana
jukumu kubwa la kumuombea Rais Dkt. John Magufuli kwani kazi anazozifanya bila
kupewa maombi ni sawa sawa na bure.
Askofu Maimbo ametoa kauli hiyo leo
Mei 21, 2018 muda mchache alipomaliza kufanya mazungumzo ya faragha na Rais
Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kusema wanaiona Tanzania inavyoelekea
katika neema ya kipekee licha ya changamoto zilizopo.
"Kuna mambo mengi mema
yanafanyika changamoto zipo. Changamoto zikiwepo zinakuonesha neema ya kuwepo,
sisi tunamuombea Rais Magufuli kwasababu kazi anayofanya bila ya maombi ni bure
kwa hiyo kazi yetu kama Kanisa kwanza ni kuomba naye, kumsimika na kumsimamisha
lakini pia na kumshauri yale ambayo yanapaswa kushauriana hasa katika maeneo ya
changamoto", amesema Askofu Maimbo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu
Mkuu Mteule wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Maimbo Mndolwa, Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais Magufuli anapaswa aombewe - Askofu Maimbo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment