Biashara ya kuwauza watanzania nje yatua Bungeni


Serikali imesema itawachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara wanaojihusisha na usafirishaji wa watanzania kwenda nje ya nchi kufanya kazi endapo itabaini kuwa wanawapeleka huko kuwauza miili yao nasio kuwaunganisha katika kazi rasmi kama walivyokubaliana.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mei 21, 2018 na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Susan Kolimba Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 33 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza la Mbunge Hawa Mchafu aliyetaka kufahamu serikali imechukua hatua gani za kisheria dhidi ya wafanyabiashara wanaosafirisha watanzania hususani vijana wa kike kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanya biashara isio rasmi ikiwemo kuuza miili yao.

"Kama taarifa hiyo itajulikana kuwa ni kweli, hatua za kisheria za nchi yetu zitachukuliwa kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo lakini mpaka sasa mimi sina 'data' za aina hiyo", amesema Dkt. Kolimba.

Mbali na jibu hilo Dkt. Kolimba amesema yeye pamoja na Wizara yake watafuatilia madai ya watanzania wanaosafirishwa kwenda na nje ya nchi na kuchukuliwa figo zao kuuzwa ili wapata kuwachukulia hatu za kisheria kwa mawakala na watu wanaofanyabiashara ya kusafirisha watanzania kwenda nje ya nchi kwa kigezo cha kufanya kazi.

Biashara ya kuwauza watanzania nje yatua Bungeni Biashara ya kuwauza watanzania nje yatua Bungeni   Reviewed by KUSAGANEWS on May 21, 2018 Rating: 5

No comments: