Baraza kuu la Vijana Chadema taifa limewafukuza uanachama
wanachama Getrude Ndibalema aliyekuwa naibu katibu mkuu wa baraza hilo na
Dickson kibona aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro kwa kosa la
usaliti ndani ya chama.
Akiongea na wanahabari Patric
Ole Sosopi Mwenyekiti wa baraza hilo amesema kuwa wamefikia hatua ya
kuwafukuza uwanachama watu hao baada ya uchunguzi kufanyika na kubainisha
kuwa wana makosa ya usaliti ambapo hivyo kwanzio Leo may 21 sio wanachama wala
Viongozi wa chama hicho.
Ameeleza kuwa pia baraza hilo
limemchagua Baraka Mfilinge Mwenyekiti wa baraza hilo Mkoa wa Iringa kuwa
Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo.
Amesema wametafakari hali ya
kisiasa nchini na wameweza kugundua kuwa kuna mkwamo wa demokrasia hapa
nchini..
Pia wamelitaka Jeshi la Polisi
kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa wameshindwa kuwakamata watu waliofanya
tukio la kumpiga Mbunge Tundu Lissu na waruhusu vyombo vya
uchunguzi vya kimataifa kufanya kazi hiyo.
BAVICHA YAFUKUZA UANACHAMA VIONGOZI WAKE WAWILI LEO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment