Profesa UDSM awapa neno wataalamu

Woga wa kupoteza vyeo, kutojiandaa na wivu, vimetajwa kuwa chanzo cha wataalam wengi kushindwa kuwaandaa watu watakaorithi madaraka yao pindi wanapostaafu ama kuacha kazi

Akizungumza  leo Mei 20 na Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi, (AQRB) Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Goodluck Urassa amesema sababu nyingine ni woga wa mabadiliko

“Wengine wanaogopa kupoteza ukubwa. Wewe ulikuwa ni CEO (Mkurugenzi Mkuu) watu wanakujua kabisa wewe ndio mkubwa kumuachia mtu mwingine na wewe ukabaki hapo hapo unashindwa. Wengine ni woga tu wa mabadiliko,

wengine wivu hataki mtu wa chini apate, kuna watu hata watoto wao wanawaonea wivu,”amesema

Amezitaja njia za kufikia mafanikio katika biashara ni pamoja na kumchagua mwanafamilia lakini kama hakuna mtu wa kusaidia unaweza kuchukua mtu kutoka nje ya familia

Pia amesema kumtafuta meneja mtaalam ama ikishindikana kuuza sehemu ya hisa za kampuni kwa mtu mwingine

Mwenyekiti wa Bodi ya Wabunifu Majengo nchini, Dk Ludihija Bulamile amesema uamuzi wa Serikali wa kutumia kwa kiasi kikubwa taasisi za Serikali katika ujenzi wa miradi ya umma itaathiri sekta za umma na binafsi kwa kiasi kikubwa

“Hii ni kwa sababu sekta binafsi inashiriki kwa kasi kubwa sana kufundisha vijana wanaomaliza vyuo vikuu ili waweze kusajiliwa na bodi,”amesema

Amesema pia kampuni binafsi ndizo zinazoajiri wataalam wengi wanaomaliza vyuo, hivyo uamuzi huo utawakosesha mahali pa kujifunzia.



Profesa UDSM awapa neno wataalamu Profesa UDSM awapa neno wataalamu Reviewed by KUSAGANEWS on May 20, 2018 Rating: 5

No comments: