Ni lazima uchunguzi ufanyike - Jeshi la Polisi


Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Salum Amdani  amesema kwamba Jeshi la Polisi linasubiri taarifa ya daktari kufahamu chanzo cha  kifo cha mwanafunzi Edward Kahitwa wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kilichotokea jana.

Akizungumza Kamanda Amdani kuwa daktari ndiye atafanya uchunguzi wa mwili wa marehemu na kuongeza kuwa itachukua muda kufahamu chanzo cha kifo.

“Chanzo hatuwezi kujua kwasababu ni lazima uchunguzi wa kitaalamu ufanyike sisi tunachoweza kusema kwamba ni kweli mwili wa marehemu ulikutwa chumbani baada ya sisi kupokea taarifa tulikwenda pale tukauchukua kwa taarifa nyinginne za kiuchunguzi” 

Kamanda huyo wa Ilala amesema serikali itakuja kutoa taarifa kamili ya chanzo cha kifo hicho baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kitabibu na kuongeza kuwa kwasasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Marehemu Edward Kahitwa alikuwa ni mwanafunzi wa  mwaka wa tatu katika katika shahada ya Famasia Chuo Kikuu cha Afya na sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS), mwili wake ulikutwa chumbani katika hosteli za Chuo hicho hapo jana mchana Mei 19, 2018.
 


Ni lazima uchunguzi ufanyike - Jeshi la Polisi Ni lazima uchunguzi ufanyike - Jeshi la Polisi   Reviewed by KUSAGANEWS on May 20, 2018 Rating: 5

No comments: