Baba
Mtakatifu, Papa Francisko amemteua Padri Anthony Lagwen kuwa Askofu mpya wa
Jimbo Katoliki la Mbulu
Taarifa
iliyotolewa na leo na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican imesema Askofu
mteule Lagwen aliyepata daraja la upadri Oktoba 18, 1999, alizaliwa
Julai 5, 1967 huko Tlawi, Jimboni Mbulu mkoani Manyara
Taarifa hiyo
iliyokaririwa na Redio Vatican, imesema baada ya masomo yake ya msingi,
aliendelea na masomo ya sekondari katika Seminari Ndogo ya Sanu, Jimbo Katoliki
la Mbulu na baadaye akapata masomo ya falsafa kutoka Seminari kuu ya Ntungamo,
iliyoko Jimbo Katoliki la Bukoba.
Baada ya hatua hiyo alihamia katika Seminari
Kuu ya Kipalapala, Jimbo Kuu la Tabora ili kuendelea na masomo ya kitaalimungu
(Theolojia).
Tangu wakati
huo, katika maisha na utume wake wa kipadri kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2000,
alikuwa Paroko-usu wa Parokia ya Bashay jimboni Mbulu. Kati ya mwaka 2000 hadi
mwaka 2004 akapelekwa na Jimbo kujiendeleza zaidi katika masuala ya biashara
kwenye Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Mwanza
Kati ya mwaka
2004 hadi mwaka 2009 akateuliwa kuwa mchumi wa Jimbo Katoliki la Mbulu.
Kati ya mwaka
2009 hadi mwaka 2011 akatumwa tena na Jimbo kujiendeleza zaidi katika masuala
ya biashara kwenye Taasisi ya East and Southern Africa Management Institute
iliyoko Jijini, Arusha.
Kuanzia mwaka 2012 hadi kuteuliwa kwake leo, amekuwa ni
mchumi wa mali za Kanisa, Jimbo Katoliki la Mbulu.
Papa amteua Padri Anthony Lagwen Askofu Jimbo la Mbulu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment