Kiongozi wa upinzani nchini Kenya,
Raila Odinga amewasihi wafuasi wake wasitishe kampeni ya kususia bidhaa
na biashara za kampuni zilizohusishwa kuwa na uhusiano na chama tawala cha
Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta.
Bwana Odinga ametoa tamko hilo leo
katika sikuukuu ya Mei mosi zilizofanyika katika mji mkuu wa Kenya jijini
Nairobi.
"Tulikuwa na hasira
nyingi kwa yale makampuni yaliokuwa yanaunga mkono serikali ya Jubilee.
Tulisema ni makampuni ambayo yanatesa watu wetu, ambayo yamekataa kukubali
uamuzi wa wananchi na tukasema watu wetu wote wasusie bidhaa za kampuni hizo.
Sasa tumeshikana mkono na Uhuru, tumekubaliana kufanya kazi pamoja tusulishe
mambo, na tumeweka sasa kamati ya ushauri ya kuleta suluhu ya kudumu"
amesema Odinga.
Ameongeza "Kwa hiyo leo
hii tunatangaza tunatoa ile amri ya kususia.
Tangazo la kususia bidhaa za
wanaotajwa kuwa washirika wa chama tawala lilitolewa Novemba mwaka jana baada
ya uchaguzi mkuu ambao ulibatilishwa na Mahakama ya juu nchini humo kwa madai
kuwa ulikuwa na dosari.
Odinga awashawishi wafuasi wake kumaliza mgomo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment