Mke wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete amefunguka na kumshauri msanii Alikiba
na mkewe pamoja na Abdukiba na mkewe kuhusu suala la ugonjwa wa UKIMWI na
kuwaambia kuwa wame makini kwani ugonjwa huo ni janga na halina tiba.
Mama Salma alisema hayo usiku wa
Jumapili ya wiki hii ambapo wasanii wao walifanya sherehe za kuwatambulisha
wake zao hivyo Mama Salma wakati akitoa nasaha zake kwa wasanii hao na wake zao
aliwataka kuliogopa janga hilo la UKIMWI.
"Dunia ina maradhi, UKIMWI ni
janga, UKIMWI ni hatari hauna kinga wala tiba hivyo ogopeni sana mdudu
anayeitwa UKIMWI kuwa mwaminifu kwa mke wako na kuwa mwaminifu mume wako wote,
mkiwa waaminifu mtayaepuka haya maradhi ambayo hayana kinga wala tiba, nyinyi
wasanii kila mtu anawapenda lakini wapendeni sana wake zenu na nyinyi wapendeni
sana waume zenu" alisisitiza
Mama Salma Kikwete.
Mama Salma amshauri Alikiba kuhusu UKIMWI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment