Katika hotuba yake leo kwenye
maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Mkoani
Iringa, Rais Magufuli ameahidi kupandisha mishahara kwa kiasi kikubwa kabla
hajamaliza awamu yake ya uongozi.
''Kipindi changu cha Urais
hakitaisha kabla sijapandisha mishahara wafanyakazi. Na mimi nataka niwaeleze
kupandisha kwangu kutakuwa si kwa elfu kumi, kutakuwa kupandisha kwelikweli'',
amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameweka wazi
kuwa alitamani sana mwaka huu kupandisha mishahara lakini baada ya kuona
changamoto zilizopo ikiwemo kulipa madeni ya nyuma akaona azimalize kwanza
kabla ya kupandisha.
Pamoja na hayo Rais Magufuli
ameviomba vyama vya wafanyakazi na masharikisho yao, kuendelea kuiunga mkono
serikali ya awamu ya tano kwasababu inaongozwa na walimu akiwemo yeye mwenyewe
na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambao wote wamewahi kuwa walimu.
Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais
wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya, kwa
maandalizi mazuri ya sherehe hizo ambazo zimefanyika kwenye uwanja wa Samora
mjini Iringa.
''Nitaongeza mishahara kwelikweli'' - Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment