Shirika la Msalaba Mwekundu nchini
Kenya limesema watu takribani ya 100 wamefariki kutokana na mafuriko
yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo.
Idadi ya watu ambao wameachwa bila
makazi imekaribia robo milioni huku shirika hilo likitoa tahadhari kwamba
huenda kukazuka magonjwa yanayoenezwa na maji machafu.
Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni Tana
River na Garissa, ambapo Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Abbas
Gullet, amesema, Idadi ya walioathirika inaendelea kupanda na kwamba hatua
lazima zichukuliwe kwa haraka
Amesema maeneo ya pwani na kaskazini
mashariki mwa nchi hiyo ndiyo yaliyoathiriwa zaidi ambapo kaya takriban 42,180
zimeachwa bila makao.
Uvula zaua takribani 100
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment