|
Sembabule, Uganda. Rais Yoweri
Museveni amezungumzia suala la mgomo wa madaktari na kwa hasira amewaita wote
walioweka vifaa chini mwishoni mwa mwaka jana kuwa ni “maadui wa Uganda
wanaopaswa kuchukuliwa hivyo.”
Madaktari kote nchini waligoma kwa
wiki tatu Novemba mwaka jana wakishinikiza Serikali kutekeleza lundo la
matakwa yao ambayo ni kuboresha mishahara yao na marupurupu ya nyumba,
magari, wafanyakazi wa nyumbani na kufanyiwa mageuzi kitengo cha kusimamia afya
cha Ikulu
Masuala mengine muhimu ambayo
madaktari walihitaji ni upatikanaji wa uhakika wa dawa, huduma nzuri na
mafunzo bora kwa wanafunzi wa udaktari
Mgomo ule ulisababisha huduma za
afya kudorora nchini na wagonjwa wengi walikufa kutokana na ukosefu wa huduma
au kucheleweshewa matibabu
Mkwamo huo wa huduma za afya
ulisababisha Serikali kuingia katika mpango uliopingwa wa kuagiza madaktari
200 kutoka Cuba kuchukua nafasi za waliogoma
Lakini, akizungumza katika
maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani akiwa katika Wilaya ya Sembabule,
Museveni kwa ari kubwa alitetea uamuzi tata wa Serikali wa kuagiza madaktari
kutoka nje akiwashtumu madaktari wazawa kwa usaliti na “kuonyesha tabia mbaya
na kinyume cha taaluma”.
|
|
Museveni awashtumu madaktari waliogoma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment