Mkurugenzi mtendaji
wa halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga Peter Nyalali
amemsimamisha kazi kaimu afisa utumishi wa halmashauri hiyo Protas Dibogo
kwa kosa la kukaidi kuwarudisha kazini watendaji wa vijiji 41 baada ya serikali
kuagiza warejeshwe.
Nyalali ametoa kauli hiyo wakati wa
kikao chake na watumishi wa halmashauri hiyo ambapo, pamoja na mambo mengine
amesisitiza watendaji hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kwenye maeneo yao mara
tu watakaporejea kazini.
Hivi karibuni serikali iliagiza
kurudishwa kazini kwa watumishi wote walioajiriwa 01/05/2004, ambapo
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali
alimwagiza kaimu afisa utumishi wa halmashauri hiyo awarudishe kazini
watendaji wa vijiji 41.
Pamoja na kutolewa agizo hilo Kaimu
Afisa Utumishi Protas Dibogo hakutekeleza agizo hilo jambo lililosababisha
Mkurugenzi Nyalali kumsimamisha kazi.
"Masharti yanaonyesha
kwamba nyie mmeanza tarehe 1 mwezi 5. Yeye anapotosha hapa anasema kwamba
mmeanza mwezi wa 6. Ninamsimamisha kazi na nafasi yake atakaa Bi Asha Majid"
Nyalali.
Tarehe 01/05/2004 serikali
iliwaajiri watumishi waliokuwa wakijitolea katika maeneo mbalimbali
nchini,ambapo tarehe 20/05/2004 serikali ilitoa kibali cha kuajiri
watumishi wapya wenye elimu ya darasa la saba huku ikiwataka kujiendeleza
wawapo kazini.
Aliyewatumbua wenye elimu ya la saba atumbuliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment