Rais Dkt. Magufuli
amefunguka na kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa walikosea
sana kwa kuchagua viongozi wala rushwa na kusema hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa
ndiyo maana hata yeye wakati wa kampeni alikosa wadhamini kwa sababu wote
walinunuliwa.
Magufuli amesema hayo leo Mei 2,
2018 akiwa anaweka jiwe la msingi katika hospitali ya wilaya ya Kilolo na
kusema anashukuru sasa viongozi hao wa CCM wameanza kuchukua hatua kwa watu hao
jambo ambalo anaamini litarudisha uhai wa chama Iringa.
"Nawakumbusha wenzangu wana CCM
kwamba rushwa ni mbaya sana na rushwa Iringa ilitawala kwa sababu mlichagua
viongozi wala rushwa ila nina shukuru mmeanza kuwachukulia hatua ila jamani
rushwa ni mbaya, na inatuchelewesha na inawanyima haki wale ambao wanastaili
kuongozwa, mimi wadhamini wote walinidhamini kutoka hapa Kilolo ndiyo maana
siwezi kuwasahau na nilipoaambiwa na Mhe. Jafo kwamba kuna hospitali imekwama
tangu mwaka 2011 kwa zaidi ya miaka mitano haijapaya pesa na imesimama na
wanataka kujenga hospitalii ya wilaya kubwa na fedha zinazohitajika ni bilioni
4.2 nikasema pelekeni watu kule hawapendi rushwa ni watu wachapakazi" alisema Rais Magufuli
Katika uchaguzi uliopita, Mchungaji
Peter Msigwa alifanikiwa kutetea kiti chake huku chama chake cha CHADEMA
kikipata madiwani 14 kati ya kata 18. Kwa matokeo hayo CHADEMA kiliandika
historia ya kuongoza halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Japo mpaka sasa
madiwani kadhaa kutoka CHADEMA wamejiuzulu nafasi zao na kurudi CCM kwa kile
wanachodai kuunga mkono juhudu za serikali ya awamu ya tano na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli.
Magufuli aweka wazi walichokosea Iringa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment