Mtendaji wa
Kata ya Mwandui iliyopo mwambao wa bonde la ziwa Rukwa, wilayani Sumbawanga
mkoani hapa, Benedict Chapewa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema tukio hilo
limetokea usiku wa kuamkia leo, Mei 3
Kamanda Kyando
amesema kuwa Chapewa ambaye amewahi kuwa Katibu Mwenezi, CCM Wilaya ya
Sumbawanga, alivamiwa na kundi la watu wasiojulikana wakati akiwa anakunywa
pombe katika moja ya baa anayomiliki kijijini hapo
“Watu hao
walimmiminia risasi kwa kutumia bunduki aina ya gobore kisha kumkata kata na
mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake,” amesema
Amesema baada
ya wauaji kutekeleza adhima yao waliondoka kuelekea kusikojulikana na
hawakuchukua kitu chochote kutoka kwa marehemu au katika baa hiyo
Kamanda Kyando
amesema uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo unaendelea kufanyika na watuhumiwa
wanasakwa popote walipo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake
Ametoa wito
kwa wananchi wa mkoa huo kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani
kufanya hivyo ni ukiukaji wa haki za binadamu na vyombo vya dola vitahakikisha
vinawachukulia hatua za kisheria wale wote wanajichukulia sheria mkononi.
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Sumbawanga auawa kwa kupigwa risasi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment