Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha,
limewapiga marufuku wanawake wajawazito kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa kwa
madai vazi hilo ni alama ya ubikira kwa mwanamke na sio vinginevyo.
Hayo yamesemwa na Paroko Msaidizi wa
Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padre Festus Mangwangi wakati akiweka
mkazo juu ya tamko lililotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Isaack Amani,
wakati akiadhimisha misa ya shukrani iliyofanyika Jumapili iliyopita, baada ya
kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Francis kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo.
Kabla
ya uteuzi huo uliotangazwa Desemba 27 mwaka 2017, Askofu Mkuu Amani alikuwa
Askofu wa Jimbo la Moshi na kusema haitakiwi kwa mwanamke yeyote ambaye
anajijua ni mjamzito kuvaa shela kipindi anafunga ndoa kwa kuwa vazi hilo
linavaliwa na mwanamke asiyemjua mwanaume (bikra).
Aidha, Padre Festus Mangwangi
amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao wa kike kutunza miili yao na kuishi
maisha ya kimaadili hadi watakapopata wenza wa kufunga nao ndoa na hapo ndipo
alama ya shela itakapoonekana umuhimu wake.
"Tamko la Askofu Mkuu
linatekelezwa kwa kuwaeleza maharusi watarajiwa wanapokwenda kupata mafundisho
ya ndoa kwa katekista na baadaye padre, kuwa kama ni wajawazito basi wasivae
shela na hata wale wanaowajua wanaume pia wanashauriwa wasivae", amesema Padre Festus.
Pamoja na hayo, Padre Festus
ameendelea kwa
kusema "wanaojitambua kuwa si bikira, hawavai
shela, lakini wako wanaojificha na kuvaa shela, hii inakuwa sawa na
kudanganya".
Kwa upande mwingine, Padre
Festus amesema endapo atatokea mtu akadanganya na kuvaa shela wakati
tayari anamjua mwanaume au kuwa mjamzito basi atakuwa anafanya utovu wa
nidhamu.
Kanisa lapiga marufuku uvaaji wa Shela za harusi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment