| Mwanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work akichangia damu |
| Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Maxwell Stanslaus akizungumza na Mkazi wa Arusha katika zoezi la uchangiaji wa damu lililoendeshwa ma taasisi yake.Picha na Ferdinand Shayo |
Taasisi
isiyokua ya kiserikali ya Wanaume inayojulikana kama Men At Work imeendesha
zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kinamama wanaojifungua na kupoteza damu
nyingi pamoja majuruhi wanaonusurika na ajali na kufikishwa katika
hospitali ya mkoa ya Mount Meru .
Mkurugenzi wa
Taasisi hiyo Maxwell Stanslaus amesema kuwa wameamua kuwa wameamua
kuchangia damu kama mchango wanaume kujitoa kwa ajili ya jamii na
kuisaidia jami kwasababu wanaume ni nguzo ya familia,jamii na taifa kwa ujumla.
Max aliwataka
wanaume wote nchini kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika kutatua
changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii .
“Kwa
sasa tumeamua kushirikiana na kitengo cha damu salama kuchangia damu ili
kupunguza changamoto ya upungufu wa damu katika benki ya damu “ Alisema Max
Max alisema
kuwa taasisi hiyo ina kazi kuwa ya kuwahasisha wanaume kuwa wawajibikaji na
kushiriki katika nafasi za malezi familia na jamii ili kujenga familia
imara na hatimaye taifa imara.
Kwa upande
wake Mwanachama wa Men At Work Rodgers Nelson alisema kuwa anajisikia faraja
kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya kinamama wajawazito ambao
hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
Naye Shemeji
Melayeki alieleza kuwa ni mara yake ya kwanza kutoa damu hivyo amewatoa
hofu wananchi kutokua waoga wa kuchangia damu kwani zoezi hilo linafanyika kwa
umakini na halina madhara yoyote.
TAASISI YA WANAUME YAJITOLEA KUTOA DAMU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment