Rais John Magufuli
amemteua Waziri Mkuu wa zamani, Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere kuwa Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa, CCM (NEC).
Hata hivyo
taarifa hiyo iliyotumwa saa nane usiku wa kuamkia leo Mei 25, na
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ilizua mjadala kwa baadhi ya
wanasiasa na wadau wa masuala ya siasa kuhoji mamlaka ya Msemaji wa Ikulu na
yale ya Ofisi ya Itikadi na Uenezi ya CCM
Mwenyekiti wa
Kamati ya Uongozi ya CUF, upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif
Sharif, Julius Mtatiro, amesema kitendo cha Msemaji wa Ikulu (Mtumishi wa
Serikali) kutangaza vikao vya CCM na uteuzi wa wajumbe wa vikao vya CCM ni
hatari
“Watanzania
wanalazimishwa kukubali kuwa watumishi wa Serikali ni watumishi wa CCM. CCM ina
msemaji wake lakini mambo ya CCM yanatangazwa na Ikulu.” amesema
Mtatiro ahoji mamlaka ya Msigwa Ikulu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment