Katika
kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM), kimeandaa mdahalo wa wanataaluma huku Rais mstaafu wa Afrika
Kusini, Thabo Mbeki akialikuwa kuwa mgeni rasmi
Mada kuu
katika mdahalo huo utakaofanyika Mei 18, 2018 na kuwahusisha wanataaluma
kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini pamoja na viongozi wastaafu na
walioko madarakani ni hali ya elimu katika Afrika
Akizungumza na
waandishi wa habari leo Jumamosi Mei 12, 2018 mjini Dodoma, Makamu Mkuu wa chuo
hicho, Profesa Egid Mubofu amesema mhadhara huo ni mwanzo wa mihadhara
itakayokuwa inafanyika kila mwaka chuoni hapo kwa ajili ya kumbukumbu ya
Mwalimu Julius Nyerere
Amesema chuo
hicho kitakuwa kinafanya mihadhara mbalimbali ya kitaaluma
Amesema Mbeki
ataambatana na mkuu wa chuo hicho, Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin
Mkapa ambaye siku za hivi karibuni alipendekeza kufanyika kwa mdahalo wa
kitaifa kujadili sekta ya elimu nchini.
Mkapa, Mbeki kutikisa mdahalo wa elimu UDOM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 12, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 12, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment