RAISI MAGUFULI TUSAIDIE WANANCHI WA KIJIJI CHA KINKO KATA YA LUKOZI TUMEUZIWA MAENEO YA SERIKALI ZAIDI YA EKARI 40
Wananchi wa kijiji cha Kinko kata ya Lukozi wilayani
Lushoto mkoani Tanga wameiomba serikali ya awamu ya Tano kuwasaidia kurejeshewa
maeneo ya mashamba ya serikali yaliouzwa kwa matajiri wachache kwenye eneo hilo
likiwemo eneo lililoko nyuma ya ofisi ya Chama cha mapinduzi.
Akizungumza mmoja wa mzee ambaye ni mzawa wa eneo hilo
ambaye alitaka jina lisitajwe amesema kuwa kuanzia miaka ya 1960 maeneo hayo
makubwa ambayo yalikuwa ni mali ya Serikali yaliuzwa kimya kimya bila wao kujua
walishangaa watu wanayalima bila taarifa kutoka kwa viongozi.
Amesema kuwa aliyehusika kuuza maeneo hayo ni mwenyekiti
aliyemaliza muda wake ambaye ni Bwana Shabani Mweri ambaye aliuza mashamba ya
kijiji ,na maeneo yote ya maji (vitivo)ambapo kwasasa kijiji hicho kimebakia na
maeneo machache tu.
Ameongeza kuwa eneo la mashamba ya kijiji yalikuwa zaidi
ya Ekari 40 lakini mpaka kufikia sasa kuna ekari ambazo hata hazizidi 22 baada
ya maeneo mengine kuuzwa.
“Kipindi hicho maeneo kweli yalikuwa makubwa lakini
bwana mweri akawauzia matajiri tajiri wa hapa kijijini kina mzee Saidi
Mdoe,Kina Ibrahimu ,na watu wengine kutoka nje ya hapa sasa tunauliza mwenyekiti
anapata mamlaka wapi ya kuuza maeneo?”Alisema mzee huyo
Hata hivyo amesema wanamtaka mkuu wa wilaya ya Lushoto
Mh Januari Lugangika kwa kuwa ndiye muakilishi wa raisi afike katika kijiji
hicho na wako tayari kuonyesha maeneo yaliouzwa na mwenyekiti aliyemaliza muda
wake bwana Shabani Mweri
Naye mmoja wa mwananchi katika eneo hilo amesema kuwa
baadhi ya watu walijaribu kufuatilia na kuhoji kuhusu maeneo yaliouzwa lakini
walibaki kutishiwa maisha na wengine kuishia polisi kwa kesi za kusingiziwa.
“Kweli bwana watu walijitokeza kupiga kelele
lakiniwalishia kuonekana wao ndiyo wabaya akiwemo mtendaji ambaye yupo kwasasa
amepambana mpaka wamepelekana mahakamani lakini matajiri wakatoa rushwa na
kupewa maeneo ambayo kwasasa wanayamiliki na sisi kama wananchi tunaogopa”Alisema
“Tunajua Raisi huku hawez kufika mana ana majukumu mengi
lakini anawasaidizi wake kama mkuu wa wilaya aje atusimamie tupate haki yetu
tuliodhulumiwa na watu wachache jamani kwanini lakini , tunataka maeneo yetu
tunamuamini raisi magufuli”Aliongeza
Hata hivyo tulizungumza na aliyekuwa mwenyekiti wa
kijiji hicho Bwana Charles Mavoa na kukiri ni kweli maeneo mengi yameuzwa
lakini kwa nfasi yake alipambana lakini hakuweza kwasababu hakupata uungaji
mkono wowote.
Naye mwenyekiti wa sasa katika kijiji hicho bwana Kirua
Mhina amesema bado kwa nafasi yake wanashirikiana kujua ni namna gani ya
kurudisha maeneo hayo yaliouzwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.
Pamoja na hayo tulizungumza na mkuu wa wilaya ya Lushoto
Bwana Januari kuhusu malalamiko hayo nakusema kuwa anapanga ziara rasmi katika
maeneo hayo ili waone ni jinsi gani ya kupata ukweli wa malalamiko hayo ya
wananchi.
Juhudi za kumtafuta mwenyekiti aliyehusika kuuza maeneo
hayo Bwana Shabani Mweri zinaendelea na kupitia muandishi wako endelea
kufuatilia zaidi Kusaganews
RAISI MAGUFULI TUSAIDIE WANANCHI WA KIJIJI CHA KINKO KATA YA LUKOZI TUMEUZIWA MAENEO YA SERIKALI ZAIDI YA EKARI 40
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment