Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema katika
kujenga uchumi wa viwanda bado Serikali inatakiwa kutazama upya sheria na sera
Akizungumza leo Mei 25, 2018 jijini Dodoma katika mkutano wa
kuhamasisha ushiriki wa wazawa katika uchumi wa viwanda, Waziri Mhagama amesema
anasimamia kikamilifu suala hilo
Amesema kila sheria inayopita bungeni amekuwa akiuliza
maudhui ya ushiriki wa wazawa kwenye sheria yenyewe ama kwenye kanuni
“Kwa sababu msingi ukiwekwa katika sheria ni lazima kanuni
itafsiri jambo hilo vizuri. Sisi kama Serikali utayari wetu ni mkubwa
sana,”amesema
Amesema dhana ya ushiriki wa wazawa itakapotekelezwa katika
miradi mikubwa inayofanywa na watu kutoka nje ya nchi lazima Watanzania
watapata ujuzi
“Ninaiona Tanzania mpya kupitia mkakati Local content
mnaokwenda kuitayarisha. Naisubiri kwa hamu. Sera za namna hii zikitekelezwa zitachangia
kukuza viwanda na makampuni ya ndani ya nchi yetu,”amesema Mhagama
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC),
Being’I Issa ambao ndio waandaaji wa mkutano huo wakishirikiana na Taasisi ya
Uongozi amesema bado bidhaa zinazouzwa kwa wawekezaji nchini ni chache
Pia amesema ushiriki wa wazawa wengi katika miradi mikubwa
bado ni kwenye ujuzi wa chini na hivyo kutaka kujengewa uwezo
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi
Nchini, Joseph Semboja ametaka uwezeshaji wa wazawa ili waweze kunufaika na
fursa zinazotokana na miradi mikubwa nchini.
Mhagama ataka sera, sheria zitizamwe upya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment