Idara ya wagonjwa Mahututi katika hospitali ya rufaa
Bugando, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa, vifaa tiba
ikiwa na sehemu finyu ya kupokelea wagonjwa zaidi ya 100 ambao wamekuwa
wakifikishwa katika idara hiyo kila siku
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Dkt. ABEL MAKUBI Ameeleza
changamoto hizo wakati akipokea hundi ya shilingi milioni 240 iliyotolewa kama
msaada na benki ya CRDB nchini kwa ajili ya kuunga mkono upanuzi wa ujenzi wa
idara ya wagonjwa mahtuti, katika tukio lililohudhuriwa na maaskofu wakuu
watatu wa majimbo makuu ya Songea, Dodoma na Mwanza
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi mkuu wa benki ya CRDB
ESTER KILEO amesema benki hiyo imekuwa na ushirikiano mkubwa na hospitali hiyo
katika kuboresha mazingira ya utoaji tiba, na hii ikiwa ni mara ya pili katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita ambapo mwaka 2013, benki hiyo ilifanya
ukarabati wa wodi ya wazazi, kutoa vifaa mbalimbali vya tiba pamoja na kupanda
miti zaidi ya 100, msaada uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 55
Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa
Bugando, ambaye pia ni Askofu mkuu wa jimbo kuu la Mwanza Mhashamu YUDA THADEI
RWAICHI ameipongeza benki hiyo kwa utayari na ushiriki wao katika masuala ya
huduma za kijamii na kwa moyo wao wa matendo ya huruma na wema katika
kumhudumia mwanadamu kimwili.
Idara ya wagonjwa Mahututi Bugando yakabiliwa na upungufu wa Madaktari
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment