Mbunge CCM amwaga chozi bungeni


Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Jacqueline Ngonyani  ‘Msongozi’ ametoa chozi bungeni akiitaka Serikali kuwalipa mawakala wa pembejeo na kuacha kutumia kivuli cha uhakiki wa madeni hayo kutoyalipa

Akichangia bajeti ya kilimo, leo Mei 15, 2018 bungeni, Msongozi amesema madai hayo yamedumu kwa zaidi ya miaka minne huku baadhi wakifariki kabla hawajalipwa

“Nashangaa sana mawakala wa pembejeo wanadai miaka minne, walihudumia wakulima wetu na walikwenda kukopa fedha katika taasisi, ambazo sasa zinawadai,” amesema Msongozi

Huku akishangiliwa na wabunge, Msongozi amesema, “Serikali imekuwa inajificha katika kichaka cha uhakiki, kwa nini hawawalipi? Serikali imekwenda kujificha katika uhakiki, ni uhakiki wa aina gani? Kuna watu wanakufa bila kupewa fedha zao.”

Msongozi akizungumza kwa sauti yenye kuashiria kulia huku mkono wake akiupeleka kufuta uso wake, amesema, “katika nchi hii watu wanatafuta haki zao, kama wameiba kwa nini wasipelekwe mahakamani, kwa nini hawapewi fedha zao, uhakiki gani, mbona watumishi siku mbili walihakikiwa? Kwa nini huku katika mawakala hawalipwi fedha zao.”

Amesema kuna kijana alitaka kujinyonga kwa kudaiwa na taasisi jambo ambalo amesema Serikali ichukue hatua ya kulipa madai kwani wako mawakala saba wamepoteza maisha.”

Msongozi amekuwa mbunge wa tatu kutoka CCM kutokuunga mkono bajeti hiyo akitanguliwa na Richard Ndassa (Sumve) na Mashimba Ndaki (Maswa Magharibi

Mbunge CCM amwaga chozi bungeni Mbunge CCM amwaga chozi bungeni Reviewed by KUSAGANEWS on May 15, 2018 Rating: 5

No comments: