Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi),
James Mbatia amewashauri viongozi mbalimbali nchini, kuutumia wimbo wa Taifa
kuongoza ili kudumisha umoja
Mwenyekiti huyo wa
NCCR-Mageuzi, ametoa ushauri huo leo bungeni Mei 22, 2018 katika mjadala
wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2018/19.
Katika mchango wake, Mbatia amegusia
mazingira yasiyo rafiki ya utalii na mikakati isiyoonyesha mwanga ya kuutangaza
ndani na nje ya nchi, huku akisema asilimia 98 ya mapato yanayotokana na utalii
yanatoka mikoa ya kaskazini mwa Tanzania
“Kuna kiongozi nilimsikia akisema
watu wa kaskazini wasubiri kwanza. Zaburi 141:3 inasema ‘Ee
Mwenyezi-Mungu ukilinde kinywa changu, uweke ulinzi mlangoni mwa mdomo wangu’,”
amesema Mbatia
Amesema kama asilimia 98 ya mapato
ya utalii yanatoka mikoa ya kaskazini, inapaswa kujengewa uwezo ili iendelee
kuwa juu
“Mama Tanzania anatuasa kuwa wamoja.
Taifa hili ni moja, watu wengine wanaotoka Kaskazini tusianze kugawana kwa
ukabila na ukanda. Tanzania ni yetu sote na wimbo wa Taifa unazungumzia hekima,
umoja na amani ili tuweze kukuza utalii wetu, viongozi wazingatie huu wimbo,”
amesema.
Mbatia ataka wimbo wa Taifa utumike kudumisha umoja nchini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment