Askari wanne
wa pori la akiba la Mkungunero Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma wanashikiriwa na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakituhumiwa kuomba na
kupokea rushwa ya Sh5 milioni za wafugaji wa Kijiji cha Irkiushiboir Kata ya
Makame Wilaya ya Kiteto mkoani Mnyara
Akizungumza Kamanda
wa Takukuru wilayani Kiteto, Julius Chacha amesema askari hao wamekamatwa Mei
20, 2018 wakiwa na bunduki nne aina ya SMG huku wakiwa na mifugo 200
Amewataja
askari hao kuwa ni Godfrey Matheas, Martenus Mahoka, Augustino Sadiki na
Aphrahimu Polepole
Amebainisha
kuwa baada ya mmoja wa wafugaji kuombwa rushwa na watu hao,
uliwekwa mtego na kukamatwa askari hao wakiwa wamepokea kiasi hicho cha fedha
na kwamba walikuwa na mifugo zaidi ya 200 mali ya familia saba za wilayani
Kiteto
“Mtego
huo uliwekwa kabla ya askari hao kuikabidhi mifugo kwa wenyewe. Tuliwakamata
wahusika wakiwa wameshikilia mifugo hiyo katika kitongoji cha Ilchura
kijiji cha Irkiushiboir wilayani Kiteto,"amesema Chacha.
Askari wanne wadakwa na Takukuru wakidaiwa kupokea rushwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment