Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG), Dk Adelardus Kilangi amesema Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla hajavunja sheria wala kanuni alipofuta vibali vya
vitalu vya uwindani
Dk Kilangi
ametoa kauli hiyo leo Mei 22, 2018 bungeni wakati akijibu hoja za baadhi ya
wabunge ikiwemo kamati ya Bunge ya Ardhi, Utalii na Mazingira waliomtuhumu Dk
Kigwangalla kuvunja sheria kwa kuvifuta vitalu 18
“Waziri
(Dk Kigwangalla) hakuvunja sheria alipochukua hatua hizi na imeelezwa vizuri
katika barua ya Januari na mawasiliano mengine ya Oktoba na Desemba, alikuwa
anachukua ili kuweka mfumo mzuri wa uendeshaji wa vitalu ili Taifa liweze
kunufaika zaidi,” amesema Dk Kilangi
Mwanasheria
huyo amesema Julai mwaka, 2017, Bunge lilitunga sheria ya usimamizi wa
rasilimali za nchi, “Lakini ilikuwa ni kuhusisha Ibara ya 9 na 27 za Katiba ya
Tanzania. Sehemu hii ya Katiba inahitaji sheria kuweza kuzitekeleza na
mheshimiwa waziri hakuvunja sheria yoyote.”
Hata hivyo,
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema, “Haya
yanayojitokeza ni kipindi cha mpito. Siwezi kusema waziri amevunja sheria au
hajavunja ninachoweza kusema ni kipindi cha mpito, ushauri wa AG utabaki kama
ulivyo.”
Kuhusu mifugo
kukamatwa inapoingia hifadhini, Profesa Kabudi amesema, “Hili ni suala nyeti,
suala zito na Serikali imelisikia jambo hili na kulizingatia. Kesi nyingi ziko
kwa Mkurugenzi wa Mashtaka na alipokea kesi zote.
AG asema Kigwangalla hajavunja sheria kufuta vitalu vya uwindaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment